Historia
Ya Miti Ya Mikarafuu Visiwani Zanzibar.
Kutokana
na historia inaonyesha mikarafuu ilianza kupandwa au kuoteshwa katika visiwa
vya Ushelisheli,Mauritius na sehemu nyengine.
Ama
mikarafuu ilioteshwa katika visiwa vya Zanzibar hii inaelezwa kuwa
ililetwa kutoka sehemu za Visiwa vya Indonesia,mashariki ya mbali,ilifika huko
Madagasca na shelisheli na kuingia Zanzibar karne ya kumi na tisa (19) na
ikaanzwa kupandwa ama kuoteshwa wakati wa ufalme wa sultani wa Oman.
Miche
hiyo ya iliyoingia visiwani humo mnamo mwaka 1818 na kuenezwa katika visiwa vya
Unguja na Pemba katika upandaji wake na ilistawi vyema na inatoa asilimia 80% ya
karafuu zinazohitajika duniani na kwa muda mrefu sasa uchumi wa visiwa vya
Zanzibar unategemea sana zao la karafuu.
Wakati
huo baada ya kupandwa kwa mikarafuu upepo wa kimbunga ulipiga na kung’oa
mikarafuu mingi kukalazimika kufanya juhudi mpya za kupanda
mikarafuu mipya na hili likawa si jambo la hiari bali ilikua lazima kwa watu
,kazi hio ilisimamiwa na utawala wa kifalme wa kisultani uliokuepo wakati huo
maarufu utawala wa sultani wa Omani.
Wataalamu
wanatueleza kuwa mti wa mkarafuu ili uwaze kumea na kustawi vyema unahitaji
sana maeneo yenye baridi kwa hivyo utaona mara nyingi
mikarafuu imeoteshwa na kustawi vizuri katika maeneo yayaliyonyanyuka maarufu
sehemu za vilima na mabonde kama inavyojulikana kuwa sehemu hizo huwa ni sehemu
za baridi na unyevunyevu kwa vipindi virefu katika mwaka.
Hata
hivyo maelezo haya hayamaanishi kuwa sehemu za tambarare hazina uwezo wa
kuotesha miti ya mikarafu ila mara nyingi mikarafuu yake inakuwa dhaifu haikuwi ikawa
mikubwa sana na pindi litatokea jua kali kwa kipindi kirefu basi ni rahisi
kuona mikarafuu imeathirika na kuaza kunyauka na baadhi yake inakufa
kabisa.
Pia
inaelezwa kwamba miti hii kama itapandwa katika ardhi iliokuwa ina rutuba nzuri
huweza kuanza kuzaa inapofikisha miaka mitano ama ikiwa ilipandwa katika ardhi
iliokuwa haina rutuba nzuri huwa inaanza kuzaa zaidi ya miaka mitano kimo chake
kinakuwa kidogo sana na hii hupelekea kutoa mazao kidogo sana.
Mikarafuu
ni miti ambayo inahitaji ushughukiaji wa hali ya juu kama vile mtu
anavyoshughulikia familia yake kwa vile shamba ni lazima lisafishwe ili miti
wenyewe iwe katika hali nzuri ili iweze kutoa mazao mazuri , hii ni kwa sababu
miti hii ni miti ambayo kiuhalisia haihimili msongamano wa miti mingine na
ikiwa hivyo basi pia uzaaji wake unakuwa dhaifu na inatoa karafuu kidogo sana,
Iko
miti miba yanye kutambaa ambayo inajulikana kwa jina la Mikekewa,
minyambonyambo miti yenye kutambaa hivyo hutambaa na kuenda juu ya mkarafuu
kuuzunguka mkarafuu wote hapo hata kama utatokea kuzaa inaathiri katika
uchumaji wake kwa sababu karafuu zote huwa zinashikwa na mkekewa na
kupururuka na kudondoka chini na huku mchumaji akishambuliwa na miba ya
mikekewa ambayo mara nyengine humpasua na kumsababishia vidonda.
Kwa
hakika mikarafuu zao pekee ambalo watu wa visiwa vya Zanzibar wanajipatia
mapato kwa wingi wale waliodiriki kuwa na mashamba ya miti hiyo,ingawaje hata
wale wasiokuwa na mashamba ya mikarafuu wanafaidika wakati wa kipindi cha
uhumaji wa karafuu kwa vile wale wenye mashamba lazima watafute wasaidizi wa
kuzichuma karafuu zao.
Karafuu
sio kama mazao mengine haziliwi na wala hazifanywi kinywaji kama matunda
mengine bali pamoja na hivyo zina matumizi mengi mfano wa hayo ni:
1.Hutumika
katika utengenezaji wa sigara.
2.Hutumika
katika utengenezaji wa dawa ya meno.
3.Hutumika
kama kiungo (spice ) katika mapishi kama chai ,pilau, n.k.
4.Hutumika
kama dawa ya maradhi ya tumbo la kuendesha,kifua.
5.Mafuta
yake hutumika kuchulia misuli na viungo vya mwili
Mnazi
kipato cha mkulima na serikali . Na ndipo hapo ninakuwa na shaka na mkulima wa minazi kumuona kuwa ni yatima hana mzazi wala mlezi. Minazi mingi iliyopo imetokana na mashamba ya kurithi ambayo huenda tumerithi toka kwa wazee wetu ama mara baada ya harakati za ukombozi wananchi kujimilikisha kama matunda ya uhuru. Kutokana na umri mrefu na kutoboreshwa mashamba kutokana na uwezo duni au tamaa za wenye mashamba kwa kuangalia mavuno bila kutahadhari uboreshwaji wa zao hilo kwa kukuza miche mipya na uwekaji wa mbolea , zao hili limejikuta siku hadi siku likiwa linatokomea. Miaka ya 80 hadi 90 zao hili lilikuwa likishughulikiwa na Mradi wa Kitaifa wa Kuendeleza Zao la Mnazi , vipi iwezekane kutoa wataalamu kuwezesha kubadilishwa zao moja kwenda lengine na kusiwezekane kutoa wataalamu wa kuendeleza na kuboresha zao lililopo. Ushauri wangu kwa wizara husika hasa ya kilimo na mazingira,jaribuni kufanya utafiti kujua jinsi gani ya kuokoa utowekaji wa zao la mnazi na pia ili serikali ijiridhishe haina budi kuchukua uzoefu wa nchi nyengine mfano wa Sri lanka , kwani kisiwa hichi kinafaidika sana na zao la Mnazi. Ukitazama athari iliyopo ni kuwa,zao la mnazi likiboreshwa litanyanyua kiwango cha maisha kwani nazi hutumika sana kwa mapishi,kutoa mafuta na ni kiburudisho cha koo na uboreshwaji wake utanyanyua uchumi kwa nchi na wananchi .
Zao la Mnazi ni alama kuu katika ukanda wa pwani ya Afrika Mashariki na ukiangalia kwa makini kutokomea kwake ni sawa na kuondoa meno halisi na kuyabadili kwa meno bandia.Kutokana na umri mrefu na kutoboreshwa mashamba kutokana na uwezo duni au tamaa za wenye mashamba kwa kuangalia mavuno bila kutahadhari uboreshwaji wa zao hilo kwa kukuza miche mipya na uwekaji wa mbolea , zao hili limejikuta siku hadi siku likiwa linatokomea. Miaka ya 80 hadi 90 zao hili lilikuwa likishughulikiwa na Mradi wa Kitaifa wa Kuendeleza Zao la Mnazi , vipi iwezekane kutoa wataalamu kuwezesha kubadilishwa zao moja kwenda lengine na kusiwezekane kutoa wataalamu wa kuendeleza na kuboresha zao lililopo. Ushauri wangu kwa wizara husika hasa ya kilimo na mazingira,jaribuni kufanya utafiti kujua jinsi gani ya kuokoa utowekaji wa zao la mnazi na pia ili serikali ijiridhishe haina budi kuchukua uzoefu wa nchi nyengine mfano wa Sri lanka , kwani kisiwa hichi kinafaidika sana na zao la Mnazi. Ukitazama athari iliyopo ni kuwa,zao la mnazi likiboreshwa litanyanyua kiwango cha maisha kwani nazi hutumika sana kwa mapishi,kutoa mafuta na ni kiburudisho cha koo na uboreshwaji wake utanyanyua uchumi kwa nchi na wananchi . Zao la Mnazi ni alama kuu katika ukanda wa pwani ya Afrika Mashariki na ukiangalia kwa makini kutokomea kwake ni sawa na kuondoa meno halisi na kuyabadili kwa meno ya bandia.
No comments:
Post a Comment